MCHUNGAJI
alitangaza siku ya kuchangia pesa ya ujenzi wa kanisa. Waumini walijitokeza kwa
wingi na kufanya changizo na kupatikana shilingi laki moja, na hapo MC
aliwakamua kwelikweli.
Mchungaji
alishukuru kwa kupata kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya ujenzi. Ghafla waliingia
majambazi sita na kuliteka kanisa. Hakuna aliyetoka na kuwataka kila mmoja
kutoa pesa aliyonayo.
Majambazi
yalikusanya huku wakawatisha kwa mapanga.
Waumini
walitoa pesa zote ambapo zilipatikana shilingi milioni moja cash!
Pesa hiyo
wakamkabidhi mchungaji na kumwambia achanganye na zilizochangwa kwa hiari.
Jumla
ikawa milioni moja na laki moja na kumwambia zote zikatumike kwenye ujenzi na
baada ya zoezi hilo majambazi yalitoka huku yakiwataka waumini kuendelea na
ibada.
Je,
hapa ni nani alikuwa na dhambi? Kati ya waumini waliochangia laki moja kwa
ajili ya ujenzi na kusema hawana pesa au majambazi waliochangisha mchango na
kupata shilingi milioni moja?
No comments:
Post a Comment