Msichana
wa kazi alitaka mama mwenye nyumba ampandishie mshahara.....Mama mwenye
nyumba akamwambia msichana ampe sababu tatu za kutaka kupandishiwa
mshahara.
Msichana:sababu ya kwanza Napika vizuri kuliko wewe.
Mama: Nani kakuambia?
Msichana: Baba kaniambia.
Mama: ok. Sababu ya pili?
Msichana: Napasi nguo vizuri kuliko wewe
Mama: Nani kakuambia na hili?
Msichana: Baba pia kaniambia
Mama: ok, na sababu ya tatu?
Msichana: Najitahidi kitandani kuliko wewe.
(Hapa mama kaonekana kutaka kujua zaidi na akawa tayari kujiandaa kumrukia akate kichwa cha binti mara moja)
Mama: Mme wangu kakuambia na hili pia?
Msichana: Hapana ni house boy kaniambia mimi najitahidi kitandani kuliko wewe.
Mama: Tafadhali punguza sauti baba yako asisikie. Nitakupandishia mshahara wako mara tatu.
No comments:
Post a Comment