mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Thursday, January 16, 2014

NIMEZIWASHA NJITI ZOTE MAMA



Mtoto mmoja alitoa kali ya mwaka baada ya kutumwa na mama yake aende dukani akununue kiberiti. Baada ya kurudi nyumbani, mama yake alimuuliza:
MAMA: Umeisha nunua hicho kiberiti?
MTOTO: Ndiyo mama.
MAMA; Umehakikisha ni kizima?
MTOTO; Ndiyo mama, nimezijaribu njiti zote zimewaka.
MAMA; Haa! Mwanangu sasa tutawashia nini kama umewasha njiti zote?
MTOTO: Mama ningejuaje kama njiti ni nzima bila kuziwasha?
Mh! Mama alikosa cha kuzungumza akabaki kutikisa kichwa.

No comments:

Post a Comment