Jamaa mmoja alipita mbele ya nyumba yetu mkononi amebeba mtoto, kutokana na mvua zinzoendelea kunyesha kukawa kuna madimbwi ya hapa na pale, jamaa akajaribu kuruka dimbwi moja bahati mbaya akateleza na kuishia mzima mzima kwenye
dimbwi, nimemsifu sana alivyojitahidi mtoto asiumie, ila yeye mwenyewe tope tupu na anachechemea. Mtoto ndio amefanya wengi tuliokuwepo hapo tukimbie tukachekee pembeni maana mtoto akang'ang'ania,
'Baba baba rudia tena'
No comments:
Post a Comment