mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Thursday, January 23, 2014

WEZI WENGINE NJAA KWELI..! EMBU CHEKI HUYU ALIVYOPATIKANA

Kuna mwizi aliingia nyumba flani kuiba, mwenye nyumba alikuwa ni hohehahe kupindukia kiasi
ambacho hakuwa na shati wala tshirt, maisha yake yote alikuwa anashinda kifua wazi. mwizi baada ya kuingia ndani akakosa cha kuiba, lakini pembeni aliona chungu kilikuwa na unga wa muhogo. jamaa akaona sio haba bora achukue chochote; akavua shati lake akalitandika chini akasogea kwenye chungu cha unga ili aumiminie kwenye shati alilolitandika chini ili aubebe kirahisi bila kuondoka na chungu, kumbe mwenye nyumba anamuona.
Jamaa alivyogeuza mgongo tu kuchukua chungu, kwa kasi ya umeme mwenye nyumba aliliiba lile
shati na kurudi chumbani fasta, mwizi aliporudi alipolitandaza shati hakulikuta, akaguna kwa sauti Mmmh!
Mke wa mwenye nyumba akamuuliza mumewe; kama naskia kuna mwizi, mume akamwambia mke hakuna mwizi tulale tu!
 Mwizi akapiga kelele hapana mwizi yupo mbona shati langu silioni!!

No comments:

Post a Comment