"Jamaa mmoja alikuwa na hisia za mapenzi kwa binti mmoja siku nyingi sana. Lakini hakuweza
kujieleza, siku moja akajikakamua kumuandikia binti message "I love you so much tafadhali
nijibu hisia zako"! Baada ya muda mfupi simu yake ikaingia sms, nguvu zikamuisha kwa kutaka
kujua binti kajibu nini, akaamua kulala asome sms kesho labda angepata ujasiri wa kuifungua
sms. Siku iliyofuata jamaa akaamka mapema akafagia uwanja, akafanya usafi nyumba nzima
na kazi zote hadi watu wakamshangaa. Mwishowe akaoga na kupata muda wa
kupumzika na kujitupa kitandani kwa shauku ili asome ile sms aliyojibiwa....ile kufungua sms tu
akakuta imeandikwa....."Hauna salio la kutosha kutumia huduma hii, bonyeza....."!!!!
No comments:
Post a Comment