Jamaa alimkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia, akamuuliza shida, yule mdada akasema maisha yamemshinda anaona heri ajiue.
Jamaa akamwambia kuwa yeye ni baharia kwa hiyo akikubali atamuweka kwenye boksi
kisha atamficha kwenye meli yake na wataweza kusafiri mpaka Ulaya wakifika huko atamuoa.....
Bibie akaona heri hilo akaingia kwenye boksi jamaa akambeba na kweli mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli...
Jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe
analala huko kwenye hako kastoo akikonga nyoyo na yule mwanamke na
kujivinjari naye huku akizidi mhakikishia mdada kuwa wanakaribia visiwa
vya comoro then wataingia Ulaya!!!!
Kisha akatoka na kuendelea na shughuli zake...
Zikapita wiki nne ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo
hicho, alipoulizwa akalazimika kueleza kila kitu, na kuwa anamuomba
nahodha asimtupe baharini bali amlinde mpaka watakapofika Ulaya....
Nahodha akamwambia mdada,
"Wala usipate taabu, ila jamaa yako kakudanganya hii si meli ya kwenda
Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni, tukifika huko we shuka.... Pole
kwa kushinda humu siku zote hizo!!!"
No comments:
Post a Comment