mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Tuesday, February 11, 2014

OHOOO..! UMEMEZA SOKSI YANGU

Siku ya harusi ilikuwa inakaribia, lakini bwana harusi na bibi harusi wote walikuwa natatizo
kubwa sana la siri, kila mmoja kichwa kinamuuma itakuwaje ndoa ikiianza. 

Bwana harusi akaenda kwa baba yake;
BWANA HARUSI: Baba ninatatizo nitafanyaje?
BABA: Tatizo gani mwanangu?
BWANA HARUSI: Baba nina tatizo miguu yangu inanuka sana si mke atanikimbia baada ya wiki
BABA: Uwe unaosha mara kwa mara harufu itatoka.
BWANA HARUSI:Baba hujui,harufu ni mbaya sana
BABA: Basi uwe unavaa soksi daima...jamaa akaona hili linaweza likanisaidia. Bibi harusi naye akaenda kwa mama yake;
BIHARUSI: Mama nina tatizo kubwa nikiamka asubuhi mdomo wangu unanuka mume si' atanikimbia?
MAMA: Kila mtu akiamka asubuhi mdomo unanuka hilo si tatizo.
BIHARUSI: Mama huelewi domo langu linanuka unaweza
kufikiri panya kafa
MAMA: Basi ukiamka asubuhi usifungue mdomo mpaka upige mswaki kwanza...
Wapenzi hawa wakaoana na kila mmoja akashilia ushauri mambo
yakawa poa.Siku moja baada ya miezi mitatu, mume aliamka asubuhi
akagundua soksi moja imevuka, akahangaika awahi
kuipata kabla mkewe hajaamka, bahati mbaya
mke akaamka;
MUME: Samahani umenionea
soksi?
MKE: Hapana,......mara harufu
mbaya ikaenea,
MUME: Ohoo masikini umemeza
soksi yangu....

No comments:

Post a Comment