Mtoto: Mama hivi binadamu walitoka wapi?
Mama: Mungu alimuumba Adam na Hawa wakazaa watoto wakaujaza ulimwengu.
Mtoto akamsubiri baba yake,,baba aliporudi zake toka kwenye kilevi mtoto akamuuliza baba yake.
Mtoto: Baba hivi binadamu walitoka wapi?
Baba: Binadamu wametokana na nyani, miaka ikapita wakawa binadamu. Mtoto akarudi kwa mama yake.
Mtoto: Mama we ulisema binadamu wameumbwa na Mungu, baba kasema binadamu wametokana na nyani inakuwaje?
Mama: Kila mtu kaongelea chanzo cha ukoo wake ndio maana nyingine hiyo.
No comments:
Post a Comment