mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Thursday, February 27, 2014

WABONGO NOMA SANA

Wabongo noma....
Mbongo mmoja alikwenda sauna (kuoga mvuke) na rafiki zake wawili, mmoja mzungu na mwingine mjapani.
Wakati wakiwa wanaoga ukasikika mlio fulani kutoka katika mwili wa mzungu. Mbongo akauliza
"nini hicho? mzungu akamwambia hiyo ni micro chip iliyo kwenye bega langu inanipa taarifa. Mbongo
akashangaa sana lakini hakutia neno. Baada ya muda kidogo ukasikika mlio mwingine wa tofauti. Mbongo na mzungu wakaulizana "nini hicho? Mjapani akasema hiyo ni micro chip iliyo kwenye kwapa langu inapokea signal toka katika setelite. 

Baada ya muda kupita mbongo akaenda chooni. Wakati alipokuwa akirudi nyuma akawa anaburuza toilet paper iliyokuwa imemng'ang'ania sehemu ya haja kubwa. Mzungu na Mjapani
wakamuuliza vipi mwenzetu, nini hicho? Mbongo akawajibu "napokea fax" 

Mjapani akazimia kwa mshangao

No comments:

Post a Comment