JAMAA mmoja alimuaga mkewe mlokole kuwa anaenda semina ya wiki moja mji
mwingine, kumbe anataka kwenda kunyoosha mgongo na kichenchede chake. Mke
akamwambia mumewe tupige magoti tusali, wakapiga magoti
MKE: Ee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake
MUME: Emen
MKE: Mpe nguvu katika yote atakayofanya huko
MUME: Emen
MKE: Akitaka kufanya uzinzi ashindwe
MUME:....(kimya)
MKE: Akifanya uzinzi apatwe na ugonjwa ya zinaa au afumaniwe
MUME:...(kimya)
MKE: Yaani akifanya uzinzi afie huko huko ili niishi kwa amani
MUME: Maombi gani hayo ya kishenzi basi siendi semina sasa furahi wewe..!
No comments:
Post a Comment