Msomi
mmoja mwenye PHD pamoja na kijana mmoja ambaye hakubahatika kwenda
shule walisafiri pamoja kwenda kutembelea mbuga moja maarufu yenye maua
na ndege wa kuvutia.
usiku ulipofika wakaweka hema lao zuri na la kisasa na wakalala usingizi mzito kabisa.
Masaa machache baadae, Yule kijana asiye msomi akamwamsha yule msomi na kumwambia:”angalia angani na niambie nini unaona ?”
Jamaa mwenye PHD akajibu:”Naona mamilioni ya nyota na mbalamwezi” Yule kijana asiye msomi tena akauliza “Unajifunza nini ukiona hivyo?”
Yule msomi akatafakari kwa dakika kadhaa kisha akajibu:
“kiunajimu inaonyesha kuwa kuna fursa nyingi sana katika hii dunia kwetu wanadamu.
Kwa upande wa muda inaonyesha ni usiku wa manane na pia kwa upande wa
imani inadhihirisha kuwa Mungu ni muweza wa vyote na sisi kwake ni
viumbe wadogo sana na tusio na mamlaka.
Kwa upande wa wanahewa ni kwamba kesho itakuwa siku nzuri sana. Kwa upande wako wewe inakuambia nini?”
Yule jamaa asiye msomi akakaa kimya kwa muda na kisha akasema: “Kiuhalisia Inaniambia mimi kuwa
”Hema letu limeibiwa!!
No comments:
Post a Comment