Tuesday, March 18, 2014
HUYU JOGOO WA NANE SASA NAMNUNUA
MKULIMA
mmoja alikuwa anafuga kuku wa kienyeji. Alikuwa na majike 36 na jogoo
mmoja. Baada ya kuona jogoo amekuwa mzee akaamua kununua jogoo jipya.
Ile jogoo mpya kufika tu kukawa na mazungumzo kati ya jogoo mzee na jogoo mgeni;
JOGOO MZEE: Karibu dogo, karibu sana nadhani tutashirikiana vizuri ili kuhakikisha hawa kuku wanataga mayai kwa wingi.
JOGOO DOGO: Wewe umeshazeeka ndio maana nimeletwa mimi damu mpya. Hakuna cha kushirikiana wala nini umekwisha wewe!
JOGOO MZEE: Kama unaona nimekwisha basi tufanye mashindano unipime
JOGOO DOGO: Mashindano gani?
JOGOO MZEE:
Tushindane mbio tuzunguke nyumba mara mbili, ukishinda mi najitoa. Ila
kwa kuwa mi mzee naomba uniache nianze kama hatua kumi mbele
JOGOO DOGO:
Poa sana hiyo haya anza kukimbia... mbio zikaanza, walizunguka nyumba
mara moja tu, mkulima akamfuata JOGOO DOGO akamkamata na kumchinja huku
akilalamika
MKULIMA: Yaani dunia imeharibika, huyu Jogoo wa nane sasa namnunua badala ya kufukuza majike analeta ubasha hapa. Yaani Museveni yuko sawa kabisaaaa..!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment