Familia moja
ilikuwa na bibi yao mzee sana aliyekuwa na matatizo ya moyo, hivyo wakawa na
makubaliano na daktari mmoja awe anampitia na kumcheki hali mara kwa mara. Bibi
akamwamini sana daktari. Siku moja Bibi akawatuma wajukuu zake wakamnunulie
tiketi ya bahati nasibu, tiketi ikashinda zawadi ya kwanza ya shilingi milioni
mia moja. Ndugu wakafanya kikao, wakawa na wasiwasi Bibi akipata habari za pesa
hizo anaweza akashtuka akafa, hivyo wakaona wamwombe ushauri daktari, ambaye
baada ya kusikiliza akawaambia wamwachie yeye atajua namna ya kumwambia Bibi
bila kumshtua. Daktari akamwendea Bibi.
Daktari: Shikamoo Bibi
Bibi: Marahaba dokta wangu, mbona leo umekuja ghafla bila ya kunitaarifu?
Dokta : Hahahahaha Bibi nataka nikuulize swali moja, kwa mfano umecheza bahati
nasibu ukashinda shilingi milioni mia moja utafanya nini?
Bibi: Hahahaha, kwanza nitakata nusu nikupe wewe maana unanisaidiaga
sana....
DAKTARI AKAANGUKA AKAZIMIA
ndugu pale wakajiuliza..! mbona kazimia yeye badala ya bibi
No comments:
Post a Comment