mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Sunday, March 16, 2014

SASA NDIYO NAENDA KUMTOA MKEO

 Jamaa alikuwa kwenye kibajaji mitaa ya mwenge akapita nje ya bar moja yenye guest house, si akamuona mkewe akipotelea ndani ya hiyo guest na kidume kingine....
Jamaa baada ya kutahamaki akapaniki....
JAMAA: "Dreva simama.... Unataka laki tatu ya chapchap?
DEREVA: "ndiyo mzee wangu."
JAMAA: "Nimemuona mke wangu kavaa ushungi wa njano kaingia kwenye ile guest, picha yake hii, ingia mtoe tena umlete hapa ukiwa unamtandika vibao wakati mi napiga simu polisi na kwa mapaparazi"
Dereva akaingia guest na baada ya dakika chache akatoka anamburula mwanamke kwa makonde.
JAMAA: "Dah! mbona umekosea, huyo siyo mke wangu umeshaharibu mambo"
DEREVA: "Najua! Huyu ni mke wangu, naye nimemkuta huko ndani, sasa ndiyo naenda kumtoa mkeo...."

No comments:

Post a Comment