mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Tuesday, April 15, 2014

UNGEKUWA HUENDI KUCHUKUA MASOMO YA JIONI UNGEMJUA



Jamaa alianza kujisifu sana kazini kwake;
makwaya: Wiki ijayo nafanya mtihani, ni miezi sita sasa nafanya masomo ya jioni, nimejua mengi sana, we unamjua John hanning speke?
mbongo: Hapana simjui
makwaya: Huyo ndie mzungu wa kwanza kuliona Ziwa Victoria, ungekuwa unasoma masomo ya jioni ungemjua huyu.
makwaya akawa kero kazini kwa maswali yake.
makwaya: We unamjua Arexander graham Bell?
mbongo: Hapana simjui
makwaya: Huyo ndie alikuwa mtu wa kwanza kutengeneza simu, ungekuwa unaenda kuchukua masomo ya jioni ungemjua.
Siku moja mbongo akamwita makwaya
mbongo: makwaya unamjua juma krosi kumi?
makwaya: Hapana
mbongo:
Huyo ndie mchepuko wa mkeo kwa miezi sita sasa, ungekuwa huendi kuchukua masomo ya jioni ungemjua
makwaya: enheeeeee..!


No comments:

Post a Comment