JAMAA kamuaga mkewe kwamba anakwenda kumsalimia mama yake anaumwa.basi jamaa akafunga safari siku ya ijumaa kuelekea kwa mama. ilipokufika jumapili jamaa akarudi na mzigo wa ndizi,viazi na misosi mingne.
MKE: mama anaendelea?
JAMAA: mama anaendelea vizuri na nilimpeleka hospital tukarudi mpaka naondoka nilimuacha karejea katika hali yake ya kawaida. mke akamwambia jamaa, Naomba hiyo mizigo uipeleke kule jikoni
jamaa kufika jikoni kamkuta mama yake ambaye ndiyo aliyedai kwamba alikwenda kwake kumjulia hali ndiye anandaa chakula! unajua kilitokea nini?
No comments:
Post a Comment