Mwalimu mpya wa Historia kabla ya kuanza kufundisha alitaka kuwapima uwezo wanafunzi kwa Kuwauliza swali kama ifuatavyo.
Mwalimu: Eeehe.. Ni Nani Aliyemuua Chifu Mkwawa?
Mwanafunz 1: Aka Siyo Mimi..!
wa 2: Wallah...Sihusiki..!
wa 3: Kwanza Me Jana sikuja Shule!
Mwalimu Alipoona Wanafunzi Wote ni wajinga kabisa akaamua kumuita mkuu wa
Shule aje kushuhudia ujinga wa wanafunzi wake,akampa lile swali mkuu wa
shule ili akawaulize wanafunzi, Mkuu Wa Shule Alipoenda akawauliza Lile
Swali "kwa vitisho" Mambo Yakawa Vile vile. Ndipo Alipomuita Mwalimu
Pembeni na kumnong'oneza "Lakini una uhakika muuaji yupo darasa hili?"
No comments:
Post a Comment