Jamaa aliingia salon na mtoto, alipomaliza kunyolewa
nywele na ndevu akamwambia kinyozi "Mnyoe na mtoto nakuja namtafutia
viatu duka la hapo jirani''. Baada mtoto kunyolewa yalipita masaa matatu
bila jamaa kurudi.
Kinyozi: Dogo vipi baba yako amekusahau nini?
Mtoto: Siyo baba yangu yule, aliniona nje akanambia tuingie hapa tutanyolewa bure
lakini mimi simfahamu.
No comments:
Post a Comment