Mdada alienda kwa mtaalamu amuangalie mambo yake maana
aliona mumewe ameanza kupunguza mapenzi. Baada ya kujieleza, mganga akatoa
Laptop yake akaunganisha intanet kisha akaanza kugugo. Baada ya dakika kadhaa
akiwa anaongea mwenyewe na kuonekana akiperuzi fesibuku na twira akainua
kichwa;
MTAALAM: dada, tatizo lako nimeliona linahitaji fedha kiasi
cha laki na nusu.
MDADA: He jamani hela yote hiyo ya nini?
MTAALAM: Mama mambo yamebadilika sana, siku hizi ili
kuwasiliana na mizimu lazima uwe na intanet sasa mimi hapa nimeweka WIFI na ni gharama maana ili
ku'skype na mizimu inaweza ikanichukua hata wiki kumpata muhusika. Sasa hapo
hiyo hela mama ni ya kulipia internet tu ili kupata maelezo ya matibabu yako
MDADA: Mzee nimeshindwa mimi.
No comments:
Post a Comment