Mshkaji mmoja alikuwa anaendesha gari katikati ya mjini,akakutana na bango kubwa (tangazo) lililoandikwa ‘Nunua mafuta ya gari yako na pata wa kulala na umtakaye kwa siku bure.’
Mshkaji kwa kiwewe
akakata kulia na kwenda katika kituo cha mafuta alichoelekezwa. Baada ya kujaza
mafuta akamuuliza mhudumu kuhusu kulala na amtakaye bure bila kuchelewa akapewa
rundo la tiketi na kutaka achague moja. Kwa hasira akachagua 3.
Mhudumu: Umekosa, jaribu tena siku nyingine.
Kwa muda wa mwezi
mzima jamaa akawa anapitia katika kituo hicho cha mafuta na kujaribu bahati
yake bila kufanikiwa.
Mshkaji: Nyie matapeli sana, mwezi huu kila siku nimekuwa nikija
kujaza mafuta katika kituo hiki, lakini sijafanikiwa kupata wa kulala naye
bure... inaelekea nyie ni wasanii tu!
Mhudumu: Wala sisi sio wasanii, inategemea na bahati ya mtu, kama
huamini nenda kamuulize mkeo maana yeye mwezi huu tu ameshashinda mara Kumi na
mbili..!!
No comments:
Post a Comment