JOHN: Mke wangu ananidharau sana
NGONGO: Kivipi?
JOHN: Anasema eti hakuna mtu mjinga kama mimi duniani
NGONGO: Huyo mama hajaona wajinga nini? Ona, ngoja nimuite
yule dereva wa kibajaji ndio ujue duniani kuna wajinga. ngongo akamuita yule
dereva wa kibajaji
NGONGO: Aise hebu chukua hizi shilingi elfu mbili, nenda pale
kwangu kaangalie kama nipo
KIBAJAJ: Ndio mzee.. Dereva akaondoka huyooo
NGONGO: Unaona John sasa ndio ujue kuna watu wajinga bwana
JOHN: Kweli yule mjinga, ningekuwa mimi ningechukua hela
halafu ningekupigia simu nikuulize kama upo
No comments:
Post a Comment