Jamaa alikuwa anapita kijijini akakuta ajali, akakuta Trekta lililokuwa limepakia magunia ya mahindi lilikuwa limepinduka na kuna kijana alikuwa anajaribu kuyasogeza magunia kutoka katikati ya barabara, akiwa amechoka kabisa
JAMAA: Pole bwana, si ungepumzika kidogo
KIJANA: Hapana baba hawezi kufurahi
JAMAA: Huyo baba yako pia ni binadamu, hebu pumzika unywe
maji kidogo
KIJANA: Baba hawezi kufurahi kabisaa
JAMAA: Acha hizo huyo baba yako kwani anadhani we mtumwa?
Hebu yuko wapi nizungumze nae
KIJANA: Yuko chini ya magunia.
No comments:
Post a Comment