mambo

mambo

WEKA

WEKA

SULUM

SULUM

Pages

Thursday, January 15, 2015

KUMBE MKE WANGU ANAFANYA BIASHARA YA NGURUWE


Jamaa alikuwa bar anakunywa, rafiki yake akaja wakawa katika mazungumzo;

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu

JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu

RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana

JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi' naita huu ni usaliti wa ndoa.

RAFIKI: Nini tena?
JAMAA: Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?

JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’  Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

No comments:

Post a Comment