Sunday, August 21, 2016
.."KUMBE MUME WANGU UMETOKA NJE YA NDOA MARA 5 TU..!
Leo mama mmoja alikua anafanya usafi chumbani kwake akakuta kisanduku kidogo, akakifungua na kukuta mayai matano na shilingi milion moja...
Aliporudi mumewe akamuuliza..."Hichi kisanduku ni cha nn pamoja na mayai..?" Mume akajibu kuwa amejiwekea utaratibu kila akitoka nje ya ndoa ananunua yai moja na kuliweka humo..
Mke wake (huku akitabasamu) akasema.."kumbe mume wangu umetoka nje ya ndoa mara 5 tu toka tuoane miaka 5 iliyopita, kumbe waliokua wakisema wewe mhuni walikua wanatuchonganisha, vp kuhusu hizo milion 1?"
Mume akajibu, "Huwa nayauza mayai pindi yanapokua mengi na pesa naweka humo..."
Mke kazimia hapa tunampepea aamke...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment