Baada
ya kutibiwa kwa muda mrefu katika hospitali ya wenye matatizo ya akili, hatimaye
madaktari wakaona kuwa Mwaki kapona, wakamuita kwa ajili ya usaili wa mwisho.
Akaulizwa ukitoka hapa utafanya nini? Mwaki akajibu, ‘Ntaenda kutengeneza
manati halafu ntakuja kuvunja vioo vyote vya hospitali yenu hii’ Hapo hapo
akarudishwa hospitali. Baada ya miezi sita akarudishwa tena kwenye usaili
matokeo yakawa yaleyale. Aliporudishwa hospitali tena, mgonjwa mwenzie
akamuuliza kwani wamekuuliza nini, Mwaki akaelezea mkasa mzima mwenzie
akamwambia usiwe unajibu hivyo we wajibu mambo mazuri watakuachia. Ilipokuja
zamu ya Mwaki kusailiwa tena alifika akiwa mpole na mtulivu, usaili ukaanza
tena.
DOKTA: Mwaki ukitoka hapa utafanya nini?
MWAKI: Kwa kweli nikitoka
hapa nitaenda kutafuta kazi kisha nitengeneze maisha yangu halafu nitafute
mwanamke nimuoe
DOKTA: Safi sana kwa kweli naona kabisa wewe
umepona. Je una mpango gani baada ya hapo?
MWAKI: Nitahakikisha
namnunulia mke wangu nguo nzuri na mwisho nitamnunulia chupi, nitautoa mpira wa
chupi moja halafu nitatengeneza manati, kisha nitakuja kuvunja vioo vyote vya
ki'hospitali chenu hiki.
No comments:
Post a Comment