Jamaa alifungwa Miaka mitano, Alipofunguliwa Akarudi Kijijini Kwao Baada Ya Siku
Mbili Akamwomba Mwenyekiti Wa Kijiji Aitishe Mkutano Maana Alikuwa Na Neno La
Kusema. Watu Wakahudhuria Jamaa Akakaribishwa Kuongea. Akachukua Sime Lake
Lililokuwa Limenolewa Vizuri, Akasimama Na Kuanza Kutoa Hotuba
MFUNGWA: Wote Mnajua Nilifungwa Miaka Mitamo Sasa Nimerudi.
Jambo La Kusikitisha Ni Kuwa Wakati Niko Jela Kuna Mtu Akamchukua Mke Wangu Na
Kumfanya Wake. Sasa Kwa Vile Yuko Hapa Mi Naua Halafu Narudi Jela. Baada Ya
Kusema Vile Akanyanyua Sime Na Kuanza Kukaribia Waliokuwa Wakimsikiliza,
Wanaume Saba Wakatimka Mbio Ghafla. Jamaa Akabaki Kaduwa, Kucheki, Kaka Zake
Wawili, Mjomba Wake, Baba Ake Mdogo, Na Rafiki Zake Watatu.
No comments:
Post a Comment