Dogo alienda kumtembelea bibi yake;
DOGO: Bibi mbona unakaa peke yako, mume wako yuko wapi?
BIBI: Mume wangu TV, ndo mana inakaa chumbani watangazaji
wanaongea na mimi kila siku.
TV yenyewe ilikuwa mbovu mpaka uigongegonge kwa ngumi ndio
picha inatoka vizuri. Siku hiyo bibi akawasha TV ikawa inasumbua akaanza
kuigonga kwa ngumi, wakati huohuo kukawa na mgeni anagonga mlango, Dogo akaenda
kufungua mlango;
MGENI: Hujambo Dogo? Bibi yako yuko wapi?
DOGO: Yuko chumbani anampiga ngumi mumewe. Mgeni akasepa
bila kuaga
No comments:
Post a Comment