JAMAA kaenda kulalamika polisi;
JAMAA: Afande nimekuja kulalamika binadamu watu wabaya sana
AFANDE: Wamefanya nini?
JAMAA: Afande huwezi kuamini, binadamu wana roho ya kinyama
isiyoweza kulinganishwa
AFANDE: Acha kupoteza muda, sema kuna nini?
JAMAA: Afande jana watu wenye roho isiyo na utu si wamekuja
gengeni kwangu na kunibambika noti feki
AFANDE: Sasa unaweza kuwatambua?
JAMAA: Afande kuna watu zaidi ya mia wanakuja gengeni kwangu
kwa siku, nitawezaje kujua nani kanipa hela feki?
AFANDE: Haya hizo noti feki ziko wapi?
JAMAA: Nimeshazitumia
No comments:
Post a Comment