Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni
jirani kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta. Mume akapandisha na kuapa
kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi. Siku walipokutana mume
kanywea maana jamaa alikuwa kajazia kifua;
MUME: Mambo jirani?
JIRANI: Mbona poa sana tu
MUME: Jirani nasikia ulimtukana mke wangu kuwa ana mdomo
kama tairi la trekta
JIRANI: Ndio
MUME: Ahahha, tairi la mbele au la nyuma?
JIRANI: La nyuma
MUME: Ahaa nilidhani ulisema la mbele, inaonekana mimi na
wewe tunawaza sawa, ila tu sijamwambia wife, si unajua akina mama wanavyoweza
kupaniki .
No comments:
Post a Comment