Jamaa alikuwa anapita kijijini akakuta ajali, akakuta Trekta
lililokuwa limepakia magunia ya mahindi lilikuwa limepinduka na kuna kijana
alikuwa anajaribu kuyasogeza magunia kutoka katikati ya barabara, akiwa
amechoka kabisa
JAMAA: Pole bwana, si ungepumzika kidogo
KIJANA: Hapana baba hawezi kufurahi
JAMAA: Huyo baba yako pia ni binadamu, hebu pumzika unywe
maji kidogo, nakuona uko hoi
KIJANA: Baba hawezi kufurahi
JAMAA: Acha hizo, huyo baba yako kwani anadhani we mtumwa?
Kokote aliko akijua ulivyofanya kazi atakubali lazima upumzike, kwani yuko wapi
saa hizi?
KIJANA: Yuko chini ya magunia.
No comments:
Post a Comment