Vuta
picha umelala mida kama alfajiri hivi... Usingizi ule wa kukesha jana
yake, halafu kuna mtu anakuja kukugongea mlangon kwa fujo sana kwenye
mida ya kama saa moja moja hivi. Ile unaamka na hasira zako kwenda
kumfungulia unajikwaa kidole cha mwisho cha mguu katika kona ya kitanda ile
ndiiii..kugeuka unaparamia ndoo za maji yanamwagika kwenye sakafu.
unafika mlangoni na maumivu ya kidole na uchovu jumlisha hasira unakutana na
jamaa anakwambia "nasajili line za simu" halafu anakutolea meno kwa
tabasamu... Eti pozi la biashara, je mtu kama huyo utamfanyaje?
..
No comments:
Post a Comment